UTUKUFU WA MUNGU
Utukufu wa Mungu ni roho ya Bwana,ni mkono wa Bwana,ni kidole cha Bwana,ni uweza wa Bwana,ni upako wa Mungu unaomwezesha mtu kutenda jaambo Fulani kupitia msaada wa Mungu.
MATH 17;1-6 Baada ya siku sita Yesu aliwatwaa petro,na yakobo,na Yohana nduguye akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani,akageuka sura yake mbele yao.Uso wake ukang`aa kama jua,mavazi yake yakawa meupe kama nuru.Na tazama wakatokewa na Musa na Eliya wakizungumza naye…………………
Wanafunzi au mitume wale watatu walichukuliwa na yesu kwa kusudi maalum la kukuza imani yao na kufahamu kuwaYesu alikuwa kweli mwana wa Mungu.Utukufu waliouona ulimfanya Petro asahau jukumu kubwa la kuubadilisha ulimwengu.Je ndugu yangu baraka za Mungu zinakufanya usahau jukumu la Mungu kwako?.Fahamu kuwa Yesu anatupitisha katika viwango mbalimbali vya utukufu wake ili atufanye watu tutakao tangaza utukufu wake hapa duniani.Cha ajabu sisi kina Petro wa leo tunataka kujenga vibanda duniani na kusahau kuwa tu wapitaji tu.Mtumishi wa Mungu kaza kamba za viatu vyako ambavyo ni utayari wa injili,mtumikie Mungu.Utakapotumika kwa uaminifu ndipo utauona ukuu wa Mungu maishani mwako na watu kuvutwa na huduma yako.
ISAYA 60;1-3 Ondoka,uangaze,kwa kuwa nuru yako imekuja,na utukufu wa Bwana umekuzukia.Maana tazama giza litaifunika dunia,na giza kuu lita zifunika kabila za watu.BALI Bwana atakuzukia wewe,Na utukufu wake utaonekana juu yako.Mataifa wataijilia nuru yako,na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako.
Katika nyakati hizi za kurudi kwa Yesu,Mungu aliahidi kubariki sana watu wake na kanisa lake.Nabii nyingi zimetoka kuwa hizi ni nyakati za roho wa Mungu kulifunika kanisa.Kama Israeli walivyoongozwa na wingu vivyo hivyo kanisa la leo linatakiwa kuonyesha utukufu wa Mungu.Wakati ulimwengu utakapokuwa kwenye giza la kiroho,matatizo,kushindwa huo ndio wakati watu wa Mungu watakapofanikiwa sana.Watumishi wa Mungu wote watakaofanya kazi ya Mungu kwa moyo watauona utukufu wa Mungu ukidhibitisha yote watakayotenda,kuwaza na kunena.
ISAYA 40;4-5 Kila bonde litainuliwa na kila mlima na kilima kitashushwa.palipoparuza patasawazishwa.Na utukufu wa Bwana utafunuliwa,na wote wenye mwili watauona pamoja kwa kuwa kinywa cha Bwana kimenena haya.
Bonde ni hali ya kitu kuwa viwango vya chini ya vipimo vya Mungu,na kilima ni hali ya kiburi au majivuno.Hivyo aliye mnyonge atainuliwa na aliye na kiburi atashushwa.Haya mawili yatakapotokea utukufu wa Bwana utaonekana kwa mtu akiyekarabatiwa na Bwana.
MAMBO AMBAYO UTUKUFU WA BWANA HUFANYA
1.Unafanya watu wafanikiwe kupitia utukufu wa Mungu Hagai 2;6-9
2.Unafanya watu wawe na hofu ya Mungu na toba la kweli Matendo 16;30-34
3.Unaleta amani na faraja ya roho mtakatifu matendo 9;31
4.Huleta mshikamano na umoja na upendo usio na unafiki. Zaburi 133;1-3.
5.Injili kuhubiriwa,uamsho kutokea na matendo ya Mungu kuonekana. Matendo 13;2-3.

No comments:
Post a Comment