Wednesday, March 11, 2009

MALEZI YAPI NI BORA KWA MWANAO?

MALEZI YA WAZAZI

MALEZI YAPI NI BORA KWA MWANAO?

MTHALI 22;6 Mlee mtoto katika njia mpasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee.

Wazazi mara zote wamekuwa wakijitahidi kutoa malezi bora kwa watoto wao,na hakuna hata mzazi mmoja anayefurahi kuona mwanae akiharibikiwa,akifeli mitihani,kupata mimba kabla ya ndoa hata kutumia madawa ya kulevya kama bangi,mirungi,cocaine n.k.
Lakini mbaya zaidi ni pale unapokuta mzazi amefanya kila analoweza kumlea binti yake au kijana wake na kumpatia kila anachohitaji lakini anakuta kile alichotumaini hakukipokea.Na inauma zaidi pale mtu wa Mungu aidha mkristo,muislamu,padre,shehe,mchungaji,askofu,kadinali au hata papa anapokuta mwanae au mtoto wa nduguye ameharibikiwa kitabia.

Swali, je malezi yapi ni bora kwa mwanao,nduguyo kijana,hata mtoto wa jirani yako?

Mtoto anapozaliwa katika familia,mara zote mambo mema hutarajiwa kwa mtoto huyo.
Wazazi huanza kupanga mipango madhubuti ya namna ya kumlea,kumvisha,kumlisha,pia kumsomesha.
Watoto wengi wanazaliwa katika familia zinazotofautiana sana.Wengine katika familia bora na nzuri ambapo hakuna uhitaji wa pesa,mavazi,chakula hata malazi.Wengine katika familia maskini sana ambapo yale mahitaji muhimu kama chakula hakuna,au hata kukutana na wali krismasi moja hadi krismasi nyingine,mavazi kununua sikukuu ya pasaka hii hata pasaka nyingine,nyumba ni full-suit,yaani aidha udongo toka ukuta hadi paa au nyasi ukuta hadi paa lakini mbaya zaidi nyumba inavuja wakati wa mvua na hakuna pa kulala wala kukaa.
Katika familia hizi cha ajabu zaidi ni pale unapokuta mtoto wa tajiri ndiye mwasilika wa madawa,mwenye ugonjwa wa zinaa kama UKIMWI,anafeli sana masomo yake darasani kuliko yule mtoto wa maskini,amepata mimba za mapema au hata kukosa adabu kabisa.

Katika upande wa pili inashangaza kuona mtoto wa maskini aliyekosa kabisa msaada naye anaingia katika msafara wa matajiri,yaani anajihusisha na ulevi,ukahaba,kutosoma kwa bidii darasani hata naye kutumia madawa ya kulevya ambayo ataombaomba kwa majirani zake watoto wa matajiri.

Nikirudi kwenye historia ya kipindi cha ukoloni,watemi ambao walitakiwa kupeleka watoto wao mashuleni waliwachukua watoto wa watumwa wao majumbani na kuwapeleka kusoma.Wakidhani kwamba kama wale watoto wangechukuliwa na wale wakoloni,basi wangekuwa sio watoto wao.Hili lilifanya wale watoto wa makabwela wasome na kuelimika na kuwa watu wenye nyadhifa kubwa.

Watoto wetu wengi siku za leo wamepoteza kabisa appetite(hamu) ya kuona kwamba wanajenga maisha yao ya baadaye.Hivyo watoto wa maskini na matajiri ndio wanaoiba mitihani ili wafaulu.Wazazi nao bado wanahonga walimu ili watoto wao wasisome bali waolewe ili wao wapate mahari.
Pia utanawazi umefanya watoto wengi wawe na mawazo ya ulaya kila siku na hilo kuwafanya kujiingiza katika tama za maisha na si kufuata utaratibu na kuacha shortcut.Wazazi wengi wanalia machozi kila siku,wamekata tamaa juu ya watoto wao.Wametafuta dawa au muarobaini kwa watoto wao bila majibu yoyote.
JIBU LA WATOTO WETU LIPO KWA YESU
MTHALI 15;1 Jawabu la upole hugeuza hasira,bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.
Yesu alipitia katika kipindi cha utotoni kama wengine,aliwatii wazazi wake,aliowasaidia kazi za useremala pia alipenda kwenda kwenye ibada za wazazi wake.
LUKA 2;52 Naye yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo,akimpendeza Mungu na wanadamu.
Tunaona maeneo yote ya yesu yalikuwa yaani yaliongezeka.Je watoto wetu wanaokua katika maeneo yote yaani,kimwili,kiroho,kiakili na hata kijamii?.
Hapo ndipo sisi wazazi tunapokosea,tunapenda sana kwenda na watoto wetu beach kuogelea tukiwa na vyupi tu.Na huu ndio tumeona uzungu na maendeleo.
Tunashikana mikono na wake zetu au waume zetu kwenda nyumba za ibada lakini tumeacha watoto wanaangalia katuni kwenye luninga na mara zote mkiondoka wanatafuta stesheni zile mnazoangalia siku zote usiku ukiwa umejifungia chumbani saa tano na saa sita usiku na mpenzio.

Lugha ndani ya nyumba,ni chombo kizuri kinachofanya watoto wakue katika mtazamo wa wazazi wao.Jiulize kama huwa hutaji matusi ya nguoni kwa mmeo eti kisa umemzoea.Hapa hata walokole msitutishe mna lugha mbaya za uani hasa kina mama.
Wokovu wenu uko wapi? Ni kwenda kanisani ibada nyingi au kunena kwa lugha?

Umepoteza maono ya mtoto kwa tabia zako na lugha zako yako na mwenendo wako mbaya.Kumbuka kwamba wewe mzazi ndiye kielelezo kwa mwanao (model).
Nakumbuka wazazi Fulani ambao wamekuwa majirani zangu ambao walikuwa na tabia ya kupigana,hasa baba anapokuta hakuna chakula.Lakini baba huyu hakuwa na tabia ya kuacha kitu chochote nyumbani au pesa za matumizi.Akifika tu na kuona jiko limenuna anaanza ugomvi na magumi na mateke.Bahati mbaya mtaa mzima waliwafahamu wazazi hawa kwa tabia ya kupigana.Hivyo hakuna aliye jishugulisha nao hata walipoona hali imekuwa mbaya sana.Mara kwa mara mama alikuwa anaondoka kwenda kwao na baada ya siku mbili anarudi tena.Watoto wao wamekuwa katika tabia hiyo hiyo ya ugomvi.

Pia yupo mtoto ambaye wazazi wake wote walikuwa na ajira nzuri na mshahara mzuri,yeye alifaulu kuanza masomo ya sekondari.Kabla hajafika kidato cha pili alipata mimba,akaacha shule.Kabla mtoto hajafikisha miaka miwili akapata mimba nyingine.Mwisho wazazi wake wakachoka na kuomba madaktari wamtoe kizazi,

MITHALI 10;1 Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye,bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye.
Kina mama mara zote huumizwa sana na tabia zisizofaa za watoto wao.Linapotokea jambo lolote baya kwa mtoto watu husema,ona linatabia kama mama yake.Tabia mbaya anasukumiwa mama,lakini mtoto akiwa na tabia nzuri watu watauliza ametokea ukoo wa nani? Hasa watoto wa kike wanapochumbiwa vijana huuliza ukoo wa yule binti ni upi,wakiangalia baba yake nani,hasa mtoto anapokuwa na tabia nzuri.Kina mama wamekuwa na uzito mkubwa sana wa malezi ya watoto, lakini kama wazazi wote wawili watashirikiana kulea watoto wao basi nina hakika wataweka mchango mkubwa sana wa malezi.Na mwishowe watoto hulelewa vizuri.Pasiwepo na hali ya wazazi kulaumiana.
VYAZO VYA TABIA ZA WATOTO KUHARIBIKA
1.MAKUNDI;
Watoto wengi wanajihusisha na makundi yasiyofaa(mob psychology) wakiwa;shuleni,nyumbani,mitaani hata makanisani.Kuwa na marafiki wabaya ni tatizo kubwa linaloharibu watoto wa leo.
Mimi ni mratibu wa shirika lisilo la kiserikali na pia mwalimu wa watoto.Nafahamu ambavyo tatizo la makundi lilivyo athiri watoto.Katika kituo changu cha kazi nimekuwa na vijana watatu ambao walikuwa watovu wa nidhamu.Kupitia vijana hawa watatu nimekuwa nikiona kama tatizo la nidhamu linaongezeka kama donda-ndugu siku baada ya siku.Nimejaribu kushirikisha kamati ya kituo changu cha huduma,tumebaki kukaa vikao na kuandika mihtasari ambayo imekuwa haina majibu.
Lakini mara zote tumekuwa tukiomba kwa ajili ya vijana hawa na kwa muda mrefu.Kijana wa kwanza kuja na kusema nataka kuokoka alikuwa muislamu kwa asili,lakini pia alikuwa na tabia ya wizi uliokithiri,yaani wizi kwelikweli si udokozi.Kijana huyu alikuwa amesifika kwa tabia hii na nimeletewa mashtaka mara nyingi kuhusu wizi wake.Nilishindwa kufanya chochote kwani niliongea naye kuhusu tabia yake hiyo lakini bado alikana kabisa kuwa yeye sio mwizi.Niliongea na mzazi wake naye anasisitiza kuwa mtoto wake ana tabia nzuri.
Mwisho nikaamua kushirikisha watu tuombe kwa ajili ya kijana huyu na wengine pia.
Tulichukua muda mrefu wa zaidi ya miezi sita kuomba kwa ajili ya kijana huyu,mpaka tukasahau kuomba tena.Siku ambayo sikupanga niliona mtoto huyu anakuja na mama mmoja wa kanisani na kusema kuwa mtoto yule aliamua kuombewa ili aache wizi pia abadilike kabisa na kuokoka.
Nilishirikisha wazee wa kanisa kuomba kwa ajili ya mtoto huyu na tangu siku hiyo alibadilika kabisa.Nilimpa siri ya kwamba ni muhimu awambie rafiki zake maamuzi yake mapya na kwamba yeye haibi tena na ameamua kuokoka na kuacha na tabia ya kuwa kibaka.Pia nilimsisitiza amwambie na mzazi wake,maana alikuwa na mzazi mmoja tu na mama yake alishafariki.Ili kwamba kama yule baba alifaidi matunda ya wizi wa mwanae basi ajue biashara imedoda,Yesu amemuweka huru kijana.
MATENDO 16;16-18
…..Kijakazi aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta,aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua……….
Unaona wazazi wengi wanafaidi kutokana na maovu ya watoto wao.Hili limefanya juhudi za kupambana na ukahaba,ulevi,madawa ya kulevya na hata uchawi zinagonga ukuta.Serikali imepiga kelele kwa habari ya ajira za watoto bila mafanikio yoyote.
Mashirika binafsi pia yamejaribu kuiunga mkono serikali lakini bila mafanikio yoyote.Sababu kubwa ni wazazi kufurahia tabia za watoto wao na makundi wanayojihusisha nayo.Ole wako umuonye mtoto wa mtu kwa tabia zake mbaya,mzazi anakuja juu kama kifaru.Usemi kuwa “mtoto wa mwenzio ni wako”ni kama umepitwa na wakati katika utandawazi.
Mashuleni adhabu za viboko zimekuwa zikipingwa,hizi zote ni tabia za magharibi kuingilia maadili yetu.Hakuna adhabu yoyote kutolewa kwa mtoto,ili mradi tu uhuru wa kufanya maovu uwepo.
Tunahitaji kuomba sana kwa ajili ya kizazi hiki cha leo kwani hakuna njia ya amani ya kushugulikia matatizo zaidi ya maombi.

2.TABIA ZA WAZAZI WAO
Kama nilivyokwisha eleza hapo juu kuhusu tabia za wazazi wengi zinarithiwa moja kwa moja na watoto wao.Mara zote sumaku huvuta kitu cha asili ya chuma,na chenye umbali Fulani.Kama uko na mwanao ndani ya nyumba basi jua hiyo ni sumaku inayovuta kila kitu toka kwako.
Yuko mzazi mmoja aliyekuwa na tabia ya kuleta wapenzi wake ndani ya nyumba.Siku moja mtoto alivutwa na ule uhusiano wa mtu wa jinsia tofauti na kutaka kujaribu akikutana na mvulana nini kitatokea.Yeye mtoto alizaliwa nje ya ndoa na hivyo akarithi ile tabia aliyokuwa akiona kwa mama yake.Siku ya siku mtoto alipata mimba na mamaye alijua,lakini alikosa ujasiri wa kusema chochote,imekuwa tabia ya kifamilia.

ZABURI 51;5 Tazama mimi naliumbwa katika hali ya uovu,mama yangu alichukua mimba hatiani.
Haya ni maneno ya Daudi,anayomwambia Mungu na kutubu.
Ukikumbuka Daudi alikuwa akichunga wakati Samweli alipokuja kumpaka mafuta mtoto mmoja wa Yese.Alipoona pembe haitoi mafuta ndipo alisema hawatokaa chini mpaka ameletwa Daudi.Daudi alikuwa amechaguliwa na Mungu kuwa mtumishi wake,lakini bado tatizo la kurithi tabia lilikuwa halijaisha kwa Daudi.

2SAMWELI 11;2 Ikawa wakati wa jioni,Daudi akaondoka kitandani akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana,wa kupendeza macho…………………

Kumbuka kuwa Daudi alikuwa amekwisha kupakwa mafuta ili kuwa mfalme.Mafuta maana yake roho mtakatifu.Pamoja na kupewa uwezo na Mungu bado alishindwa kusimama na kuepuka tamaa.Je mtu wa Mungu umewahi kujiuliza kwa nini pamoja na kujazwa roho mtakatifu bado unasema uongo? Bado mkali? Bado unatamani wake au waume za watu?.
Hiyo ni tabia ya kurithi toka kwa mababu zetu au wazazi wengi ambao walifanya mambo mabaya tukiwa wadogo na hawakujua kuwa tunajifunza toka kwao.

Daudi alichukuwa mke wa Uria na kumpa mimba na kisha kusababisha kifo cha uri vitani kwa kumuweka mstari wa mbele.Mungu alimfanya Daudi atoe gharama kubwa sana.Kila jambo la upumbavu mtu analofanya mbele za Mungu lazima alipe.

Bath-sheba alimzaa Sulemani ambaye katika maisha yake amekuwa na historia ya kuoa wake wengi.Inasemekana Sulemani alioa wake 700 na masulia 300 jumla Elfu moja.
Hii ndio hali ya kurithisha watoto tabia,anafanya uovu wa kupita nyingi kuliko uliofanya wewe mzazi.

Kama mzazi utajenga tabia njema kwa watoto wako hili litafanya mtoto wako awe bora zaidi.Kuna mfumo wa kuwawekea watoto akiba katika benki za NMB na zinginezo ambao utamfanya mtoto wako aweze kujijengea tabia ya kuweka akiba.
Pia katika hali ya chi yetu ambapo umaskini umekuwa king`ang`anizi ni bora sana tunapowajenga watoto katika hali za kukataa umaskini wao wenyewe.Wanaposoma lengo liwe kupata maisha bora kwa kuwa wagunduzi sio kuajiriwa tu.

No comments:

Post a Comment