Saturday, March 7, 2009

SHAHIDI WA YESU

SHAHIDI WA YESU
Shahidi ni mtu anayetoa ushuhuda juu ya mtu fulani au juu ya jambo fulani.
Katika mahakama shahidi mara zote anakuwa upande wa mtu anayempa-support.Ni mara chache shahidi kuwa kinyume na mtu anayemtolea ushahidi.Usemi wa shahidi,tabia ya shahidi,hata mwenendo wa shahidi unashabihiana na ule wa muhusika wa kesi.
Wakristo wengi ni mashahidi wa Yesu.Hivyo wanatakiwa kufanana na Yesu katika kila eneo la maisha yao.Sitarajii kuona mkristo yuko kinyume na Bwana wake Yesu kristo.
Kuwa shahidi wa Yesu kunatofautiana sana na ule ushahidi unaotolewa mahakamani.Ushahidi kwa Yesu unatakiwa uwe na msaada wa nguvu za roho wa Mungu na upako wa kumuwezesha shahidi kuwa kielelezo cha Yesu bila hofu.

MATENDO 1;8 Lakini mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu roho mtakatifu nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu,na katika uyahudi wote,na samaria,na hata mwisho wa nchi.
Yesu alijibu swali la wanafunzi kuhusu ufalme,yeye hakuhitaji kutoa maelezo kuhusu ufalme maana alijua kuwa ufalme wa Mungu umo katika Nguvu zake.Hivyo aliwasisitiza kuwa wao walikuwa na kitu cha msingi kupokea zaidi ya ufalme.
Mtumishi wa Mungu napenda pia kukutia moyo kuwa majibu ya maisha yako yamo katika nguvu za Mungu.Uhitaji wako uko katika kiasi cha nguvu za Mungu ulizo nazo.
Roho mtakatifu ndiye anayeleta nguvu,lakini yeye mwenyewe sio ile nguvu.Ili mtu awe shahidi ni lazima iwepo nguvu ya kumuwezesha kuonyesha ushuhuda wake,pia awe na sura,tabia na mwenendo tofauti na ule wa ulimwengu au watu wengine wenye dini lakini hawana nguvu za Mungu.

1WAFALME 20;22 Naye yule nabii akamjia mfalme wa Israeli,akamwambia,enenda ,kusanya nguvu zako ujue na kuangalia ufanyavyo,kwa maana mwakani mfalme wa shamu atakuja juu yako.
Nabii alijua kwamba hakuna msaada mwingine kwa mfalme kama nguvu za Mungu.Nabii asingemshauri mfalme akusanye bunduki na mapanga na mikuki.Bali kukusanya nguvu za Mungu.Huu ndio ulikuwa msaada wa pekee na siri ya kushinda siku zote.Je ndugu yangu unapenda kuwa mshindi kwenye kazi zako,biashara zako,ndoa yako na hata masomo yako?.Kusanya nguvu na upako wa Mungu.
Uko upako wa aina nyingi;
i.upako wa kuhubiri.
ii.upako wa mali na fedha.
iii.upako wa kuishi na mke wako kwa amani.
iv.upako wa kuimba.
v.upako wa kuombea wagonjwa n.k.

MAENEO YA USHAHIDI
1.Maisha ya kiroho. 1kor 4;1-2 Mtu na atuhesabu hivi,kuwa tu watumishi wa kristo na mawakili wa siri za Mungu.Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.
Mtumishi wa Bwana fahamu kuwa wewe ni mtu muhimu na Mungu anajua anaye mtu anayemwakilisha duniani.Katika kumwakilisha Mungu duniani fahamu kuwa huwezi bila Nguvu ya Mungu mwenyewe.Siri ya utumishi wetu ni kumiliki nguvu za Mungu tu.

2.Maisha na jamii inayokuzunguka.Ebrania 12;1-2 Basi na sisi pia kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii na tuweke kando kila mzigo mzito na dhambi ile ituzingayo kwa upesi.
Ushahidi wetu pia unachunguzwa na ulimwengu mzima,pale tunaposhindwa kumdhihirisha Yesu duniani kwa sababu ya nguvu zetu ndogo za kustahimili upinzani wa ibilisi duniani,

3.Maisha ya kiuchumi 3yohana 1;2 2petro2;9-10 kumb 8;18
Tunapokuwa mashahidi wa yesu jambo la msingi ni kujua kuwa ulimwegu unatutazama na kutaka kujifunza je Yesu tunayemtamka anaweza kubadilisha maisha yetu ya kiuchumi na kuwa mazuri.Nakumbuka watu wengi nilipookoka walivyonishangaa.Wengi walisema pamoja na kusoma kwangu nimekata tama na kuokoka ni nisubiri kufa tu.Mimi nilijua kuwa Mungu aliniokoa kwa makusudi ya kumtumikia,pia kubarikiwa naye kwa asilimia 100%.Hivyo kama umeokoka kuwa watu wataangalia afya yako,mali zako,familia yako,mke wako hata ndugu zako,je unawathamini?.Ukiwa maskini huwezi kuthamini watu kwani huna cha kuwasaidia.Msihi Mungu leo akupe mali hasa kwa ajili ya kumtumikia.

SIFA ZA SHAHIDI WA YESU
1.Anakuwa mwaminifu hata kufa ufunuo 3;20
2.Anabeba chapa za Yesu maishani mwake. Gal 6;17
3.Anaonyesha vipawa na karama za roho mtakatifu 1kor 12;4-11
4.Anaonyesha tunda la roho kwenye maisha yake. Gal 5;22

No comments:

Post a Comment