Tuesday, March 10, 2009

DARASA LA YESU LA IMANI

DARASA LA YESU LA IMANI
EBRANIA 10;38 Lakini mwenye haki wangu atishi kwa imani,nye akisitasita roho yangu haina furaha naye.
EBRANIA 11;6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu,kwa kuwa mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yupo na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

Yesu alifundisha kwa asilimia 85%,alihubiri kwa 10%,alitenda miujiza kwa 5%.
Katika mafundisho alizungumzia sana somo la imani,ambayo mara zote aliwafundisha wanafunzi wake kwa mifano halisi.

Imani ni ule uhakika wa yale yasiyokuwepo kutamkwa kana kwamba yapo,pia imani inavuta yale yaliyombali na kuyaleta karibu.
Ili tufanikiwe katika maisha yetu hapa duniani,lazima tupite katika njia ya imani,hii ndio njia aliyotuchagulia Mungu tuishi(spiritual life style).

LUKA 18;8 Je nitakapokuja duniani nitaikuta imani?.
Yesu alijibu swali la wanafunzi kuhusu maisha yao na kufanikiwa kwao, kwamba ili wafanikiwe walipaswa kuishi kwa imani mpaka Yesu atakaporudi.

Mtumishi wa Mungu jiulize swali hili,je imani waliyokuwa nayo kina Ibrahimu,isaka na yakobo,kina Musa,kalebu,Joshua Daudi,samweli na Eliya,tunaweza kujifanananisha na sisi?.Biblia inaorodhesha katika Ebrania 11 masshujaa wote wa imani.

DARASA LA IMANI LA I
MARKO 11;12-14 Hata asubuhi yake walipotoka Bethania aliona njaa,akaona kwa mbali mtini wenye majani,akaenda ili labda aone kitu juu yake,na alipoufikilia hakuona kitu ila majani maana si wakati wa tini,akauambia tangu leo mtu asile matunda kwako,wanafunzi wake wakasikia.
Yesu alijua kuwa ule haukuwa msimu wa tini.Lengo hasa lilikuwa kufundisha wanafunzi kwa njia ya vitendo.Mara zote huwa Yesu anatupitisha katika madarasa ya imani ili tukue kiroho.Je umewahi kupingwa,kukataliwa,kujaribiwa au kutengwa kwa ajili ya kumwamini Yesu?.Hayo ni madarasa ya Yesu ya kukuza imani yako.

DARASA LA IMANI LA II
MATHAYO 14;22-33 Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda nga`mbo wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano…
Yesu alipowambia wanafunzi wake kwenda ng`ambo wakati yeye mwenyewe alikwenda kuomba mlimani.Alifahamu kabisa yale yatakayotokea watakapofika katikati ya bahari.Lengo lake lilikuwa kumtumaini Yesu hata asipokuwepo.Wakati wakiendelea na safari mawimbi makubwa yalianza kukipiga kile chombo,hapo ndipo wanafunzi walianza kukosa kumtazama Yesu.Je ndugu mpendwa una tatizo hili pia? Unapokutana na mawimbi unasahau kuwa yesu yuko pamoja na wewe? Mara zote yesu anahitaji kuona ni kwa kiasi gani unamtegemea.Pia mawimbi yanapokuwa makubwa ndivyo hutokea na kutoa msaada.Lakini wengi wanaposaidiwa na uwepo wa yesu kristo,huanza kukemea pepo na kutoamini kuwa msaada huo unatoka kwa Bwana yesu.Petro alionyesha ujasiri mkuu.Hatuangalii kuzama kwa petro,lakini Petro alionyesha ujasiri wa kutembea juu ya maji.Je mtumishi wa Mungu waweza kutembea juu ya matatizo,majaribu,kupingwa na kutemewa mate kama Yesu na bado macho yako yakamtaza Yesu.Petro alifuzu darasa la Yesu kwa 95%.MATH 16;18,19 Nami nakwambia wewe ndiwe petro na juu ya mwamba huu nitalijega kanisa langu,wala milango ya kuzimu,yaani upinzani,imani potofu,imani za uongo hata dhambi hazitalishinda kanisa la yesu.Katika wanafunzi watatu waliokuwa karibu sana na Yesu,Petro peke yake ndiye aliyekabidhiwa funguo za ufalme wa mbingun

DARASA LA IMANI LA III
MARKO 4;35-40 Siku ile kulipokuwa jioni,akawaambia na tuvuke kwenda ng`ambo,wakauacha mkutano,wakamchukua vile vile alivyo katika chombo.
Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye.Ikatokea dhoruba kuu ya upepo,mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji.Naye mwenyewe alikuwa kwenye shetri amelala juu yam to………….
Tunaona Yesu anaongeza kuwakamilisha wanafunzi wake kwa kuwapitisha tena katika mawimbi.Chombo mara nyingi humaanisha maisha ya mtu,na kinavyopita katika maeneo mbalimbali kinaposafiri ndivyo kinaonyesha uhalisi wa maisha ya mtu anavyoishi hapa duniani.
Yesu kwa urahisi kabisa aliamka akaukemea ule upepo,ndugu unapaswa kumwamsha Yesu ndani yako,yupo lakini amelala.Unapomwamsha tu anaukemea ule upepo unaokutesa kiurahisi kabisa.Nashuhudiwa kuwa liko jambo linakusumbua sana,linakufanya usilale usiku,linakufanya usile chakula,linakufanya ulie machozi.Ndugu ni rahisi tu mwamshe Yesu ndani yako.Utaniuliza nitamwamshaje? Sawa,

i.Jipangie ratiba ya kusoma neno la Mungu kila siku.
ii.Jipangie ratiba ya kuomba kila siku,kwa imani bila kupiga kelele za kushidwa.
iii.Amua kuokoka kikwelikweli kama bado ulikuwa msindikizaji.
iv.Abudu na watu wanaoukiri wokovu na kutangaza habari zaYesu.

BIBLIA INASEMAJE KUHUSU IMANI
I.Ni kumtegemea Mungu kwa asilimia 100%.
II.Kuona mambo yasiyokuwapo kana kwamba yapo tayari na umeyapokea.
III.Ni ngumu kumpendeza Mungu pasipo imani.
IV.Imani ni mkono wa kupokelea baraka toka kwa Bwana.
V.Imani inaweza kukua na kuongezeka.

DALILI ZA IMANI
I.Imani inatii neno la Mungu na sheria za Mungu.
II.Imani inafanya ushirika na Mungu.
III.Imani inaziamini ahadi za Mungu.
IV.Imani inafanya mtu ajikane na mambo ya dunia.
V.Imani inleta ushindi katika upinzani.
VI.Imani inaweza kuleta mateso kwa ajili ya Yesu.