MUUJIZA WA KWANZA WA YESU
Muujiza ni tukio lisilo la kawaida linaloonyesha ukuu wa Mungu katika taratibu za kibinadamu.Pia muujiza ni tendo linalotokea nje na kanuni za kibinadamu ambalo huleta faida katika matokeo yake.
-Yesu alifanya miujiza mingi ili ;
1.kuonyesha uwezo wake wa kutawala taratibu za kibinadamu.
2.kujitambulisha kuwa yeye ni mwana wa MUNGU.
3.kufanya watu wamwamini.
4.njia aliyotumia mara zote kufundishia wanafunzi wake.
Yako maneno matatu yenye tofauti ndogo lakini yanafanana;
Ishara – huleta ushahidi juu ya jambo linaloleta upinzani.
Maajabu – ni tendo linaloleta mshangao linapotendwa.
Miujiza – ni tendo linaloonyesha muhuri wa kazi ya Mungu.
-Mtu anayetenda miujiza, maajabu na ishara,hudhihirisha uwepo na ukuu wa Mungu, pia huonyesha mamlaka ya Mungu.
-Mambo yanayotokea muujiza unapotendeka;
1.Huinua imani ya watu
2.Hudhihirisha ukuu wa Mungu.
3.Huongeza ujasiri
4.Huleta hofu ya Mungu
5.Huleta uamsho wa kiroho.
YOHANA 2;1- 11 MATEN 4;29-31 KUTOKA 7;20-21
-Yesu alifika huko kana kuhudhuria harusi ya marafiki wa familia yao maana hata mama yake Yesu alikuwepo.
-Yako mambo kadhaa tunayojifunza toka kwa Yesu;
1.Yesu pamoja na huduma ya Mungu ndani yake lakini alipenda kufika kwenye matukio mbalimbali ya kijamii.Je mara zote tunafika kwenye mambo yanayohusu jamii au tunakwepa? Je Yesu asingefika kwenye harusi ya kana ungetokea muujiza huu?.
2.Mariam alikwenda kuomba msaada kwa Yesu alipoona divai imeisha.Je sisi tunamtazama nani wakati wa kupungukiwa,shida,kuugua,majaribu n.k.
3.Yesu alitengeneza divai njema kwa kubadilisha maji ambayo hayakuwa na radha na kuwa divai safi. Je anaweza kubadilisha uchungu ulionao moyoni mwako kuwa furaha?
Muujiza mkubwa katika maisha ya mtu ni pale anapobadilishwa maisha yake kwa Yesu kuingia moyoni mwake.Je unaweza kumruhusu Yesu kuingia moyoni mwako?
Anafahamu shida yako japo hutaki kumshirikisha,Anafahamu mapito unayopitia lakini anataka umpe nafasi wewe mwenyewe kumwambia kwamba unahitaji msaada wake.
Mara nyingi umeanza kutatua tatizo wewe mwenyewe,lakini hukupata msaada.Umewambia majirani,marafiki,wataalam na waganga bado hukupata nafuu
Yoyote.Leo ndio siku ya muujiza wako je uko tayari kupokea?
4.Mariam aliwaambia watumishi, lolote atakalowaambia fanyeni.Yesu bado anatoa maelekezo yake mpaka leo, anataka mtu atii ili apokee muujiza wake.Mara ngapi Yesu amesema na wewe juu ya mwenendo wako, maisha yako, hata tabia ile ambayo huwezi kuiacha.Je lolote atakalokwambia utafanya? Je uko tayari kuchukua hatua ya imani katika maisha yako kufanya yale ambayo ufahamu wako umeshindwa?.Yote yawezekana kwake aaminiye
.
YESU BADO ANAISHI NA KUTENDA MIUJIZA MIKUBWA ANATAKA UAMINI TU. MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUCHUKUA HATUA.
No comments:
Post a Comment